Total Pageviews

Monday, December 29, 2014

Kitu Hiki Kimoja Kitakufanya Uweze Kujiajiri, Uishie Kuwa Mwajiriwa Au Uishie Jela.


Habari za jumatatu rafiki?
Tunaelekea kabisa ukingoni mwa mwaka 2014.Najua unefanikiwa mengi, umepata changamoto kwenye machache na umejifujza mengi pia.
Najua pia unajiandaa vyema kwa mwaka 2015.


Leo nataka tukumbusane kitu muhimu sana ambacho ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuzingatia.Kitu hiko ni NIDHAMU...
Unapoweza kuwa na nidhamu ya kujisimamia wewe mwenyewe yaani nidhamu binafsi unaweza kujiajiri, kuwa mjasiriamali au kufanya biashara.
Unaposhindwa kuwa na nidhamu ya kujisimamia mwenyewe utahitaji mtu wa kukusimamia na hivyo utapata mtu wa kukuajiri na utakuwa muajiriwa, ukijaribu biashara itakushinda.
Unapokosa Nidhamu kabisa, yaani huna nidhamu kabisa unaishia kukaa jela.
Fanya maamuzi mazuri mwaka 2015, jijengee nidhamu binafsi.
Kama hujui uanzie wapi ili kujijengea nidhamu binafsi jiunge na KISIMA CHA MAARIFA, tumejadili hatua kwa hatua jinsi ya kujijengea tabia hii.
Tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz na ujiunge.
Nakutakia kila la kheri.
TUPO PAMOJA.

CREDIT :  WWW.KISIMACHAMAARIFA.CO.TZ

No comments:

Post a Comment