Total Pageviews

Wednesday, February 5, 2014

NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI  

Taasisi  ya  RAFIKIELIMU  FOUNDATION  kupitia  mradi  wa   ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINI,  inatangaza  nafasi  za  MAFUNZO
YA  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI .


Wahitimu  wa mafunzo  haya  watapata  nafasi  ya  kufanya  kazi  kama  waalimu  wa  ujasiriamali  katika   MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI &  VIJIJINI.

   SIFA  ZA  MWOMBAJI :

1.    Awe  raia  wa  Tanzania  mwenye  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha   nne  na  kuendelea.
2.   Awe  mkaazi  wa  Dar  Es  salaam.
4.  Awe  na  wito  wa  kufanya  kazi  ya  ufundishaji.
5.  Awe  tayari  kufanya  kazi  kama  mwalimu  wa  ujasiriamali katika  wilaya  yoyote  ya Tanzania  bara.

MAFUNZO   yatatolewa  kwa  mwezi  mmoja   kuanzia  tarehe     10  MACHI  2014.
ADA   YA  MAFUNZO  HAYA  NI  NAFUU  SANA.

Fomu za  kujiunga  katika  mafunzo  haya  zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa  gharama  ya SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU.
Ofisi  zetu  zinapatikana  katika  eneo  la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

Kufika katika  ofisi zetu, panda  mabasi  ya  UBUNGO  kwenda CHANGANYIKENI, kisha  shuka  katika  kituo cha  TAKWIMU  halafu tembea  hatua  ishirini  mbele, utaona  bango  limeandikwa   RAFIKIELIMU   COLLEGE.

MWISHO   WA   KUCHUKUA   FOMU  ZA  MAOMBI  NI  TAREHE   28  FEBRUARY  2014..

 Wahi  fomu  yako  mapema, kwani  nafasi  zilizopo  ni  chache  sana.

Kwa   maelezo  zaidi,  wasiliana  nasi  kwa  simu  namba 0784406508.

No comments:

Post a Comment