Total Pageviews

Thursday, February 20, 2014

MAMIA YA VIJANA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA BURE YA UALIMU WA UJASIRIAMALI.

Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  kupitia  Mradi  wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  na   Vijijini  ( EUMIVI  -Project )  imejipanga  kutoa  mafunzo  ya  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI  kwa  vijana  wapatao  watano  kutoka  katika  kila  kata  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

Mafunzo  haya  yataanza  rasmi  siku  ya  tarehe  02  Machi  2014  saa  tano  kamili  asubuhi  katika  ukumbi  wa  Chuo  Cha  RAFIKIELIMU  COLLEGE  uliopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.

Akizungumza  na  RafikiElimu  BLOG, Mratibu  Msaidizi  wa  Mradi  wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  kanda  ya  Dar  Es  salaam, Ndugu   ARISTARICK  MALLYA    amesema  kuwa, lengo  la  mafunzo  hayo  ni  kuwajengea  vijana  hao  uwezo  wa  kutoa  mafunzo  ya  ujasiriamali  kwa  vijana  wenzao  waliopo  katika  kata  wanazo  ishi.

 Awamu   ya  kwanza  ya  Mradi  huu  ilianza  mnamo  tarehe  01  Septemba  2012  ambapo  sisi  kama  taasisi  kwa  kuwatumia  wataalamu  wachache  tulio nao, tulizunguka  katika  wilaya  mbalimbali  nchini  Tanzania  kwa  ajili  ya  kutoa  mafunzo  haya.

Moja  kati  ya  changamoto  tulizo  kutana  nazo, ni  uhaba  wa  waalimu  wa  ujasiriamali  nchini  Tanzania.

Sekta  ya   ELIMU  YA  UJASIRIAMALI nchini  Tanzania, inakabaliwa  na  changamoto   ya  UHABA  WA  WAALIMU  WA  UJASIRIAMALI.

Hii  ni  changamoto  kubwa  sana  ambayo  inahitaji  ufumbuzi  wa  haraka  ili  kuwasaidia   wajasiriamali  wadogo  wadogo    waliopo  katika  maeneo  ya  mijini  na  vijijini.

Kwa  kuanza  tutaanza  kutoa  mafunzo  kwa  vijana  kumi  ( 10 )  kutoka  katika  kila  kata  ya   mkoa  wa  Dar  Es  salaam.

Baada  ya  mafunzo  haya, vijana  hawa  watapatiwa  vyeti, wataunganishwa  na  kuunda  kikundi ama  taasisi  itakayo  husika  na  kutoa  mafunzo  ya  ujasiriamali  kwa  wajasiriamali  wadogo  wadogo  waliopo  katika  kata   wanazo  ishi.

Kikundi  hicho  kitaingizwa  katika  MTANDAO  WA  WAALIMU  WA  UJASIRIAMALI  TANZANIA  na  kunufaika  na  fursa   mbalimbali  zitakazo  tolewa  chini  mtandao.

Hii  ni  fursa  ya   kipekee  kwa vijana  wa  kitanzania  waishio  jijini  Dar  Es  salaam  wenye  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne  na  kuendelea.

Fikeni  katika  Chuo  Chetu  kwa  ajili  ya  kujiandikisha  katika  mafunzo  ya  bure  kabisa  ya  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI  yatakayo wajengea  uwezo  wa  kuwasaidia   kujiajiri  kama  waalimu  wa  ujasiriamali.

MAFUNZO YA BURE YA UALIMU WA UJASIRIAMALI

Taasisi  ya  RAFIKIELIMU  FOUNDATION  kupitia  mradi  wa   ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINI,  inatangaza  nafasi  za  MAFUNZO
YA  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI .

Wahitimu  wa mafunzo  haya  watapata  nafasi  ya  kufanya  kazi  kwa  kujitolea   kama  waalimu  wa  ujasiriamali  katika   MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI &  VIJIJINI.

             IDADI   YA   NAFASI  :

Nafasi 10  katika  kila  kata  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

   SIFA  ZA  MWOMBAJI :

1.    Awe  raia  wa  Tanzania  mwenye  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha   nne  na  kuendelea.
2.   Awe  mkaazi  wa  Dar  Es  salaam.
4.  Awe  na  wito  wa  kufanya  kazi  ya  ufundishaji.
5.  Awe  tayari  kufanya  kazi kwa  kujitolea   kama  mwalimu  wa  ujasiriamali  katika  kata  yoyote  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.MAFUNZO   yatatolewa  kwa  mwezi  mmoja   kuanzia  tarehe     02  MACHI  2014.
ADA   YA  MAFUNZO :  MAFUNZO  HAYA  YANATOLEWA  BURE.Ofisi  zetu  zinapatikana  katika  eneo  la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

JINSI  YA  KUTUMA  MAOMBI :

Matumbi  yote  yatumwe  kupitia barua  pepe  yetu  ambayo  ni  : rafikielimutanzania@gmail.comMWISHO   WA   KUPOKEA    MAOMBI  NI  TAREHE   28  FEBRUARY  2014..

Wednesday, February 19, 2014

MAFUNZO YA BURE YA UIGIZAJI FILAMU NA UIMBAJI

RAFIKI ELIMU   MUSIC   &  FILM  ACADEMY
·        Je  wewe  ni  kijana  wa  kitanzania?
·       Una  umri  wa  kuanzia  miaka 15  na  kuendelea ?
·       Una  ndoto za  kuwa  muigizaji filamu  mkubwa  nchini  Tanzania?
·       Una  ndoto  za  kuwa  mwanamuziki ama  muimbaji  mkubwa hapa  Tanzania ?

RAFIKIELIMU  MUSIC &FILM  ACADEMY   ni  kituo  kinachotoa  mafunzo  ya  UIGIZAJI  na  UIMBAJI  kwa  vijana wa kitanzania  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  kumi  na  tano na  kuendelea.
Wahitimu  wa  mafunzo  haya  hupata  nafasi  ya  kushiriki  katika  filamu , maigizo, tamthiliya  na nyimbo mbalimbali   zinazo  tayarishwa  na Taasisi  ya   RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

ADA  YA  MAFUNZO :  Mafunzo  haya  hutolewa BURE!

Mafunzo  yataanza rasmi  tarehe  02 MACHI  2014.

Mwisho  wa  kujiandikisha   ni  tarehe  28 FEBRUARI 2014.

Chuo  chetu  kinapatikana  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

Kufika  Chuoni  kwetu, panda  daladala za  UBUNGO-CHANGANYIKENI  kisha  shuka  katika  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele, utaona  bango  limeandikwa  RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

JINSI  YA  KUJIANDIKISHA :Tuandikie  barua  pepe  kwenda :  rafikielimutanzania@gmail.com    

Kwa  maelezo zaidi, wasiliana  nasi  kwa  SIMU 0784406508    Au  Fika  Katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.

Wednesday, February 5, 2014

NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI  

Taasisi  ya  RAFIKIELIMU  FOUNDATION  kupitia  mradi  wa   ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINI,  inatangaza  nafasi  za  MAFUNZO
YA  UALIMU  WA  UJASIRIAMALI .


Wahitimu  wa mafunzo  haya  watapata  nafasi  ya  kufanya  kazi  kama  waalimu  wa  ujasiriamali  katika   MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI &  VIJIJINI.

   SIFA  ZA  MWOMBAJI :

1.    Awe  raia  wa  Tanzania  mwenye  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha   nne  na  kuendelea.
2.   Awe  mkaazi  wa  Dar  Es  salaam.
4.  Awe  na  wito  wa  kufanya  kazi  ya  ufundishaji.
5.  Awe  tayari  kufanya  kazi  kama  mwalimu  wa  ujasiriamali katika  wilaya  yoyote  ya Tanzania  bara.

MAFUNZO   yatatolewa  kwa  mwezi  mmoja   kuanzia  tarehe     10  MACHI  2014.
ADA   YA  MAFUNZO  HAYA  NI  NAFUU  SANA.

Fomu za  kujiunga  katika  mafunzo  haya  zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa  gharama  ya SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU.
Ofisi  zetu  zinapatikana  katika  eneo  la CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

Kufika katika  ofisi zetu, panda  mabasi  ya  UBUNGO  kwenda CHANGANYIKENI, kisha  shuka  katika  kituo cha  TAKWIMU  halafu tembea  hatua  ishirini  mbele, utaona  bango  limeandikwa   RAFIKIELIMU   COLLEGE.

MWISHO   WA   KUCHUKUA   FOMU  ZA  MAOMBI  NI  TAREHE   28  FEBRUARY  2014..

 Wahi  fomu  yako  mapema, kwani  nafasi  zilizopo  ni  chache  sana.

Kwa   maelezo  zaidi,  wasiliana  nasi  kwa  simu  namba 0784406508.