Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2013

TAARIFA FUPI YA UCHUNGUZI JUU YA MATUKIO YA MIMBA KWA WANAFUNZI WILAYA YA HANDENI, MKOANI TANGA

  Baadhi  ya  wanafunzi  wakihojiwa  na  mwandishi  wa  habari  hii( hayupo pichani  ) TAARIFA FUPI YA UCHUNGUZI JUU YA MATUKIO YA MIMBA KWA WANAFUNZI WILAYA YA HANDENI, MKOANI TANGA. UTANGULIZI Uchunguzi huu umefanyika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Uchunguzi umefanyika kuanzia Machi 19, 2013 katika Kata tatu za Wilaya ya Handeni, ambazo ni pamoja na Kata ya Chanika, Kata ya Vibaoni na Kata ya Kidereko. Uchunguzi huu wa kihabari ni mwendelezo wa utafiti uliofanyika Machi Mwaka jana (2012), kuangalia ukubwa wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia (GBV), katika vipengele vya Ubakaji, Watoto wa Kike Wanafunzi Kulazimishwa Kuolewa, Vitendo vya Ukeketaji, Vipigo kwa Wanawake pamoja na Vitendo vya Utelekezaji Watoto na Wanawake. Uchunguzi wa pili umefanyika kuangalia mrejesho wa matukio ya mimba na ndoa katika umri mdogo katika maeneo hayo, ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanyika kwa utafiti wa mwaka jana. MBINU ZA UCHUNGUZI Kabla ya kuanza kwa utafiti huu Chama cha Wanah

NAFASI ZA MAFUNZO NA INTERNSHIP

                        NAFASI   ZA  MAFUNZO  NA  INTERNSHIP RafikiElimu   Foundation  ni   Taasisi   Isiyokuwa   ya   Kiserikali   ( NGO )  inayo   jihusisha   na   Maendeleo   Ya   Jamii nchini .  Taasisi   inatangaza   nafasi   za   mafunzo   ya   NGO  MANAGEMENT & OPERATION  kwa   vijana    wenye   sifa   zifuatazo : 1.         Umri   miaka   18  hadi 45. 2.       Elimu   kuanzia   kidato   cha  nne , sita na   kuendelea . 3.       Uwezo   wa   kuwasiliana   kwa   ufasaha   kwa   lugha   za   Kiswahili   na   kiingereza . 4.       Uwezo   wa   kusoma   na   kuelewa   mwenyewe   kwa   njia   ya   masafa . 5.       Uwe   mkaazi   katika   mojawapo   kati   ya   wilaya   zilizopo   Tanzania  bara . Mafunzo   haya   yatatolewa   kwa   njia   ya   posta   na   yatatolewa   kwa   miezi   mitatu . Mwezi   mmoja   ni   wa   mafunzo   kwa   nadharia   na   miezi   miwili   ni   ya   mafunzo   kwa   vitendo   ambayo   yatafanyika   katika   taasisi   zisizokuwa   za   k