Total Pageviews

Tuesday, May 21, 2013

HII NDIO KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA AJARI YA MELI YA MV BUKOBA ILIYOZAMA TAREHE 21 MAYMeli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbwi pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uhokoaji
  MV Bukoba ikiwa inazama ilikuwa ni tarehe 21 mei 1996
 
 Makaburi ya Igoma ambako ndugu zetu waliokuwa wakisafiri kwa meli ya MV Bukoba walizikwa.

RIPOTI ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.
Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.
 
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema haina dini, huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga, kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.
 
Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa mv Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa; aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.
 
Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka 2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer Feleshi.
Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita mchana.
 
Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118 iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, mv Bukoba ilizama kwa sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.
 
Serikali iliahidi kukata rufaa; lakini hadi leo majaliwa ya rufaa hiyo hayajulikani; na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia bila kujua hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.
Kwa kipindi kirefu, mv Bukoba ilikuwa ‘kaburi’ lenye kuelea katika Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa na viwango vya ubora wa kuwa majini.

Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji; ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti na ilikosa uwiano

Wednesday, May 15, 2013

NAFASI ZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MOROGORO.               
             
  NAFASI  ZA  MAFUNZO  YA  UJASIRIAMALI  MJINI  MOROGORO.
RAFIKIeLIMU   MOROGORO   wanakuletea    SEMINA  YA  MAFUNZO  YA  UJASIRIAMALI . Mafunzo  yatakayo  fundishwa  ni  pamoja  na  Utengenezaji  wa  bidhaa  mbalimbali  kama  vile  ; Sabuni  za  aina  mbalimbali,  chaki, mishumaa, usindikaji,   utengenezaji  wa  manukato (  perfumes ), lotion, mafuta  ya  kujipaka, kiwi, mango  pickles, Chilly  Sauce, Tomato  Sauce   nakadhalika.
WAPI  :  BERRICK EDUCATION CENTRE    karibu  na  SABASABA, mkabala na JENGO LA CCM MKOA MOROGORO.

 .
LINI   :  Tarehe   20    MEI   hadi  31  MEI   kuanzia  saa  nane  kamili  mchana  hadi  saa  kumi  na  mbili  jioni .
ADA  YA  KUSHIRIKI  :  Shilingi   Elfu  Kumi  Tu  ( Tshs. 10, 000/=)
Kwa  maelezo  zaidi  wasiliana  na  Uongozi  wa    RAFIKIELIMU  MOROGORO  kwa  simu :   0764524562.

Tuesday, May 14, 2013

UPDATE: WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MANZESE WAKUMBWA NA UGONJWA WA KUANGUKA


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo.


Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.

PICHA  KWA  HISANI  YA  BLOGS  MBALIMBALI.

Sunday, May 12, 2013

UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya. Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo.

Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973 wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika mwaka uliotangulia.

Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Selestine Gesimba

KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 10/05/2013

Thursday, May 9, 2013

ALBINO AFUKUZWA SHULE JIJINI MBEYA KWA MADAI KWAMBA NI MCHAWIAmina Mwamkinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo wakimtuhumu kuwa mchawi majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.

Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi wetu alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo.

katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina.

katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu
=========  ========  ============
KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.
  
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
  
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
  
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.

Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo  baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
  
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun  iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
  
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
  
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale  alisema alikuwa  halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.

Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote  kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.
 
CREDIT:  MBEYA  YETU  BLOG.
 
KUTOKA  RAFIKIELIMU  BLOG :  Tunalaani  vikali  sana  kitendo  kilicho  fanywa  na  uongozi  wa  shule   ya  sekondari  Hollywood kumfukuza  shule  binti  huyu  mlemavu  kwa  tuhuma  ambazo  chanzo  chake  ni  imani  potofu, tunampa  pole  binti  huyu  na  tunawaomba  wanao  husika  na  mamlaka  kuingilia  kati  suala  hili  ili  kumsaidia  binti  huyu  aweze  kuendelea  na   masomo  yake. Tunamuomba  Mungu  ampe  moyo  wa  subira  binti  huyu  katika  kipindi  kigumu  hiki  anacho  pitia  katika  maisha  yake.

MWENYEKITI WA BARAZA LA MITIHANI - (NECTA ) ANADAI KUWA HAYUKO TAYARI KUYABADILI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE -201


Kuna  tetesi  kwamba  Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amegomai kubadili matokeo ya Kidato cha Nne- 2012.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa.

 "Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?" alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo. 

Hata  hivyo, siku  za  hivi  karibuni  mwanahabari  wetu  alizungumza  na  Ofisa Habari wa NECTA, John Nchimbi ambaye alisema wamekwishapokea maelekezo kwa barua na kufanyia kazi ili kujitahidi ndani ya muda mfupi matokeo yawe yametoka.

Nchimbi alikiri kuwapo kwa kasoro katika matumizi ya mfumo huo mpya wa usahihishaji, kwani hawakushirikisha wadau wengi kabla ya kuanza kutumia, lakini lengo la Baraza lilikuwa jema katika kukuza elimu nchini
“Kutokana na tangazo hili, wanafunzi hawa wote hawana matokeo tangu juzi ( yalipofutwa bungeni ), hivyo wasubiri matokeo mapya yatakayotangazwa, na waelewe wazi kuwa si lazima waliofeli wafaulu wote,” alisema  Nchimbi.

--->Ngoja  tuone  hatima  ya  vita  hii  ya  WANASIASA  na  WANATAALUMA

Monday, May 6, 2013

NAFASI ZA MAFUNZO NA INTERNSHIP : MAY INTAKE

Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation   inapenda  kuwatangazia  vijana  wa  kitanzania  nafasi  za  mafunzo :KOZI  ITAKA YO  FUNDISHWA : 
    HIV/AIDS  AND  COUNSELLING FOR  WOMEN.
SIFA   ZA  MWOMBAJI  NAFASI :
1.Awe  wa  jinsia  ya kike ( Msichana/Mwanamke )
2 Awe   mtanzania    mwenye  umri  wa  kuanzia  miaka  18  hadi  45.
3. Awe   na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha sita   nakuendelea au  awe  mwanafunzi  katika  taasisi yoyote   ya  elimu  ya  juu.
4. Anayeweza  kusoma  na  kuelewa  kwa  njia  ya  masafa  marefu. 
6. Akiwa   na  ufahamu wa msingi  (  Basic  Knowledge  )  wa masuala  ya Research   atafikiriwa   kwanza.
7.  Awe  anaishi    katika  wilaya yoyote  iliyopo  Tanzania  bara.
MUDA  WA  MAFUNZO : Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  miezi  mitatu.  Mwezi  mmoja  utakuwa  ni  mafunzo  kwa  njia  ya  nadharia  na  miezi  miwili  itakuwa  ni  mafunzo  kwa  njia  ya  vitendo  ambayo  yatafanyika  mashuleni na   kwenye  vituo  vya  mafunzo ya  ujasiriamali.
BAADA  YA  KUHITIMU : Wahitimu  wa  mafunzo  haya, watapata  nafasi  ya  kuandika  kwa  pamoja    kitabu kinacho  wahusu  wanawake wa  Tanzania   naUkimwi pamoja  na  nafasi  ya  kufanya  internship  kwa  miezi miwili  katika  taasisi inayojihusisha  na masuala  ya  wanawake  na ukimwi Tanzania.
 ADA  YA  MAFUNZO: Ada  ya  mafunzo  haya  maalumu  ni  shilingi  elfu     25   tu  kwa  mwezi.
ADA  YA  FOMU   A MAOMBI :  Ada ya Fomu ya maombi  ya  kujiunga na  masomo  haya ni shilingi  Elfu  12 tu.
Tuma  maombi   ya  fomu  ya  kujiunga  na  mafunzo-kazi  haya   kupitia  barua  pepe yetu  ambayo  ni :  rafikielimutanzania@gmail.com.
Maombi  yaelekezwe  kwenda  kwa  :
Mkurugenzi  Mtendaji,
RafikiElimu  Foundation,
Centre  For  Distance  Learning  Programme.
S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.
Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe   17  MEI  2013
Mafunzo  yataanza, tarehe        21 MEI     2013.

Thursday, May 2, 2013

NAFASI ZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI ARUSHA.
               
             
  NAFASI  ZA  MAFUNZO  YA  UJASIRIAMALI  JIJINI  ARUSHA.
RAFIKIeLIMU    FOUNDATION   kwa  kushirikiana  na  Taasisi  ya    VISION  FOR  YOUTH  ya  Jijini  Arusha, wanakuletea    SEMINA  YA  MAFUNZO  YA  UJASIRIAMALI . Mafunzo  yatakayo  fundishwa  ni  pamoja  na  Utengenezaji  wa  bidhaa  mbalimbali  kama  vile  ; Sabuni  za  aina  mbalimbali,  chaki, mishumaa, usindikaji,   utengenezaji  wa  manukato (  perfumes ), lotion, mafuta  ya  kujipaka, kiwi, mango  pickles, Chilly  Sauce, Tomato  Sauce   nakadhalika.

WAPI :   KWENYE  UKUMBI  WA  MAKUMBUSHO  ULIOPO  KARIBU  NA  MNARA  WA   MWENGE.
LINI   :  Tarehe   20  hadi  21  Mwezi  wa  Tano  ( MEI )  kuanzia  saa  tatu  kamili  asubuhi  hadi  saa  tisa  kamili  alasiri.

ADA  YA  KUSHIRIKI  :  Shilingi   Elfu  Ishirini  Na  Tano  Tu  ( Tshs. 25,000/=)
Kwa  maelezo  zaidi  wasiliana  na  Uongozi  wa  Taasisi  Ya VISION FOR  YOUTH  kwa  Simu : 0762580504.
AU  Fika  katika  ofisi  zao  zilizopo  katika  eneo  la   NAIROBI  ROAD, LUSONA  HOUSE,  3rd  FLOOR