NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU WA UJASIRIAMALI. NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI ( MARCH 2013 INTAKE ) ( INTAKE HII NI MAALUMU KWA WAOMBAJI WANAOTAKA KUWA WAALIMU WA UJASIRIAMALI KATIKA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI & VIJIJINI KWENYE WILAYA WANAZO ISHI ) Taasisi ya RafikiElimu Foundation inapenda kuwatangazia vijana wa kitanzania nafasi za mafunzo na kazi kama ifuatavyo : KOZI ITAKA YO FUNDISHWA : UALIMU WA UJASIRIAMALI. SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI : 1. Awe mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45. 2.Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne, sita na kuendelea. 3. Aliye na utashi na malengo ya kufanya kazi kama MWALIMU WA UJASIRIAMALI kwenye Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini. 4. Anayeweza kusoma na kuelewa kwa njia ya masafa marefu.