Total Pageviews

Friday, December 7, 2012

BABA ADAIWA KUMPA MWANAE WA KUMZAA MWENYE MIAKA 16

 
 
 
 
Mkazi wa Mtaa wa Mbete, Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika
 
 
 
Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha
 

Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo
 
 
 
 
Mkazi wa Mtaa wa Mbete, Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.

Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa
daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.


Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe 12/12 mwaka huu.

Source: Mbeya Yetu.
 
 
 
 
 
 
Huyoooo anatoka nje ya mahakama
 
 
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
 
 
 
 
Njooni  sasa, huku  kashika  jiwe.
 
 
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku akiwa na jiwe lake mkononi
 
 
 
Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo
RafikiElimu  Foundation, tunalaani  vikali  kitendo  cha  kinyama  kilicho  fanywa  na  mwanaum  huyu. Licha  ya  kwamba  kitendo  hicho  kimelaaniwa  vikali  katika  vitabu  vyote  vitakatifu, na  kuhamaramishwa   na  sheria  za  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania, kinarudisha  nyuma maendeleo  ya  taifa  letu, kwani  binti  huyo  alipaswa  kuwa  shuleni  kwa  ajili  ya  kupata  elimu  na  maarifa  ambayo  yangeweza  kumsaidia  hapo  baadaye  yeye  pamoja  na  jamii  na  taifa  kwa  ujumla. Tunaziomba  asasi  mbalimbali za  kutetea  haki  za  wanawake  na  watoto kwa  kushirikiana  na  Wizara  ya  Maendeleo  na  Jamii , Wanawake  na  watoto  kulivalia  njuga  suala  hili  kuhakikisha, haki  inatendeka. 

No comments:

Post a Comment