Total Pageviews

Wednesday, December 12, 2012

NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI ( NGO STUDIES THROUGH DISTANCE LEARNING PROGRAMME )


Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation   inapenda  kuwatangazia  vijana  wa  kitanzania  nafasi  za  mafunzo  na  kazi  kama  ifuatavyo :

KOZI  ITAKAYO  FUNDISHWA :  NGO  MANAGEMENT & OPERATION.

SIFA  ZA  MWOMBAJI  NAFASI :

1. Kijana  wa  kitanzania  mwenye  umri  wa  kati  ya  miaka  18 hadi 45.
2. Elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  sita  na  kuendelea.
3. Aliye   na  malengo  ya  kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizokuwa  za  kiserikali  zilizopo  nchini  Tanzania.
4. Anayeweza  kusoma  na  kuelewa  kwa  njia  ya  masafa  marefu. 


LENGO  LA  KOZI  HII :i.                   kumuandaa  mhitimu   kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizo  kuwa za  kiserikali   katika  maeneo  ya    ubunifu, uandishi  na  usimamizi  wa  miradi  yenye  kuvutia  na  kushawishi  wafadhili
( Designing, Developing & Managing Donor  Funded  Projects  )

ii.                 Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  kwa  ufanisi mkubwa   katika  taasisi zisizokuwa  za  kiserikali  katika  maeneo  ya  utafutaji  na  utengenezaji  wa  fedha   za  kukuza  mfuko  wa  taasisi  husika.

(  Designing, Managing & Developing  Fund  Raising  Programmes  )


iii.              Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  kwa  ufasaha  mkubwa  katika  taasisi  zisizokuwa   za  kiserikali   kama   mtafiti  wa  tafiti  za  aina  mbalimbali  kama  vile  tafiti  za  kijamii, tafiti  za  mazingira, tafiti  za  kisheria  nakadhalika.
iv.              Kumuandaa   mwanafunzi  kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizokuwa  za kiserikali  kama  msimamizi  na  mratibu  wa   miradi  na  shughuli  mbalimbali  za  taasisi  husika.

v.                 Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  katika  taasisi  zisizo  kuwa  za  kiserikali  kama  mwalimu  wa  somo  la  ujasirimali, uongozi  wa  biashara  pamoja  na  utengenezaji  wa  bidhaa  za  aina  mbalimbali  kwa  njia  ya  nadharia  kama  vile  sabuni, chaki, mishumaa, batiki  nakadhalika.

vi.              Kumuandaa  mwanafunzi   kufanya  kazi  kama  msimamizi  wa shughuli  za   katika  taasisi  zisizokuwa  za  kiserikali  zinazojihusisha  na  masuala  ya  uwekaji  na  ukopaji  wa  pesa   ( VICOBA  & SACCOSS )  pamoja  na  usimamizi  wa  uundwaji  wa  taasisi  za  aina  hiyo.

vii.            Kumuandaa  mwanafunzi  kufanya  kazi  katika  taasisi  mbalimbali  kama  mtoa  elimu  ya  ukimwi, mazingira  na  uraia. n.k.


MUDA  WA  MAFUNZO : Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa  miezi  mitatu.  Mwezi  mmoja  utakuwa  ni  mafunzo  kwa  njia  ya  nadharia  na  miezi  miwili  itakuwa  ni  mafunzo  kwa  njia  ya  vitendo  ambayo  yatafanyika  katika  taasisi  zisizo  kuwa  za  kiserikali.

BAADA  YA  KUHITIMU : Wahitimu  wa  mafunzo  haya, watapata  nafasi  ya  kufanya  " internship "  kwa muda  wa  miezi  sita, katika  miradi  mbalimbali inayo  ratibiwa na  taasisi mbali mbali  zisizokuwa  za  kiserikali  nchini  Tanzania  kwa  kutumia  ujuzi  walioupata  katika  mafunzo  haya.

ADA  YA  MAFUNZO  : Ada  ya  mafunzo  haya  ni  nafuu  sana.
Tuma  maombi   ya  fomu  ya  kujiunga  na  mafunzo-kazi  haya   kupitia  barua  pepe yetu  ambayo  ni :  rafikielimutanzania@gmail.comm.

Maombi  yaelekezwe  kwenda  kwa  :
Mkurugenzi  Mtendaji,
RafikiElimu  Foundation,
Centre  For  Distance  Learning  Programme.
S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.

Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  08  JANUARY 2013.

Mafunzo  yataanza, tarehe  14  JANUARY  2013.

Tunapokea  maombi  kutoka  waombaji  waliopo  katika  wilaya  zote  za  Tanzania  Bara.


Friday, December 7, 2012

BABA ADAIWA KUMPA MWANAE WA KUMZAA MWENYE MIAKA 16

 
 
 
 
Mkazi wa Mtaa wa Mbete, Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika
 
 
 
Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha
 

Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo
 
 
 
 
Mkazi wa Mtaa wa Mbete, Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.

Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa
daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.


Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe 12/12 mwaka huu.

Source: Mbeya Yetu.
 
 
 
 
 
 
Huyoooo anatoka nje ya mahakama
 
 
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
 
 
 
 
Njooni  sasa, huku  kashika  jiwe.
 
 
Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku akiwa na jiwe lake mkononi
 
 
 
Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo
RafikiElimu  Foundation, tunalaani  vikali  kitendo  cha  kinyama  kilicho  fanywa  na  mwanaum  huyu. Licha  ya  kwamba  kitendo  hicho  kimelaaniwa  vikali  katika  vitabu  vyote  vitakatifu, na  kuhamaramishwa   na  sheria  za  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania, kinarudisha  nyuma maendeleo  ya  taifa  letu, kwani  binti  huyo  alipaswa  kuwa  shuleni  kwa  ajili  ya  kupata  elimu  na  maarifa  ambayo  yangeweza  kumsaidia  hapo  baadaye  yeye  pamoja  na  jamii  na  taifa  kwa  ujumla. Tunaziomba  asasi  mbalimbali za  kutetea  haki  za  wanawake  na  watoto kwa  kushirikiana  na  Wizara  ya  Maendeleo  na  Jamii , Wanawake  na  watoto  kulivalia  njuga  suala  hili  kuhakikisha, haki  inatendeka. 

Thursday, December 6, 2012

NAFASI NNE ZA KUJITOLEA WILAYA YA ILALA


   NAFASI  NNE  ZA  KUJITOLEA  WILAYA  YA  ILALA.

TUNAWEZA  WOMEN  GROUP  ni  Asasi  Isiyokuwa  ya  Kiserikali  ( NGO )  inayo  jihusisha  na maendeleo  ya  wanawake  Tanzania. Taasisi  inatangaza  nafasi  za  kujitolea  kama  ifuatavyo :

1. Mtaalamu wa ujasiria mali...NAFASI  MOJA.
2.Mtaalamu wa kukuza pesa za mfuko wa taasisi.....NAFASI  MOJA.
3. Mwalimu wa michezo................NAFASI  MOJA.
 4. Mtaalamu wa  masuala  ya  sheria  na  haki  za  binadamau............NAFASI  MOJA.

Tuma  maombi  yako  kwenda  kwa  :

MWENYEKITI  ,
TUNAWEZA  WOMEN  GROUP.
S.L.P  DAR  ES  SALAAM.

tUMA  MAOMBI  YAKO  KUPITIA  : womentunaweza@yahoo.com

WASILIANA  NAO  KWA  SIMU  : 0784399400,0715485834.

MAOMBI  YOTE  YATUMWE  KABLA  YA  TAREHE  14 DESEMBA  2012.

Monday, December 3, 2012

NAFASI ZA UFADHILI WA MASOMO YA SEKONDARI KWA YATIMA

RafikiElimu  FOUNDATION  ni  Taasisi  isiyokuwa  ya  kiserikali  inayo  jishughulisha  na  Maendeleo  ya  jamii. Taasisi  inapenda  kutangaza  nafasi  za  ufadhili  wa  masomo  ya  sekondari  kwa  waombaji  wenye  sifa  zifuatazo  :

1. Awe    yatima  wa  jinsia  ya  kike  au  awe  masichana  anayeishi  katika  mazingira  magumu.
2.Awe  raia  wa  Tanzania.
3. Awe  anajiandaa  kujiunga  na  masomo  ya  kidato  cha  kwanza  kuanzia  Januari  2013. AU
4. Awe  anajiandaa  kujiunga  na  masomo  ya  kidato  cha  tano   katika  mwaka  wa  masomo 2013/14.
5. Awe   ni  mwanafunzi  ambaye  tayari  anasoma sekondari   lakini   anashindwa/ ama  ameshindwa  kuendelea  na  masomo  yake  kutokana  na  kufiwa  na  wazazi ama  walezi wake.


*  N.B  : Ufadhili  wa  masomo  kwa  kidato  cha  tano  na  sita   utatolewa  kwa  wanao  taka  kuchukua  masomo  nya  michepuo  ya  ARTS.

Tuma  barua  yako  ya  maombi  ya  ufadhili  wa  masomo  kwenda  kwa :

MKURUGENZI  MTENDAJI,
RAFIKIELIMU   FOUNDATION,
S.L.P  35967,
DAR  ES  SALAAM.

*   Katika  barua  yako  ambatanisha  barua  ya  serikali  ya  mtaa  unaoishi, cheti  chako  cha  kuzaliwa ama  Hati  ya  Kiapo " AFFIDAVIT " , picha  zako nne  za  rangi, pamoja  na  vielelezo  vingine  vinavyo  thibitisha  kwamba  wewe  ni  yatima.

* Maombi  yako  yatufikie  kabla  ya  tarehe   07  JANUARY 2013.

*  Maombi  yanaweza  kutumwa  na  msimamizi  wa  mwanafunzi  husika  kwa  niaba  yake.