Total Pageviews

Sunday, November 11, 2012

SOMO LA PILI : UTENGENEZAJI WA MISHUMAA.


Mishumaa., Utengenezaji  wa  mishumaa  huweza  kusaidia  kuongeza  kipato  cha  mjasiriamali, kwani  bidhaa  hii  huitajika  sana  kwa  matumizi  mbalimbali  kama  vile  matumizi  ya  majumbani  nakadhalika.
 MALIGHAFI   ZINAZO  HITAJIKA  WAKATI  WA  UTENGENEZAJI  WA  MISHUMAA.

1. Paraffin  Wax
2. Utambi
3. Mould  (  Umbo )
4.  Stearine  au  mixture
5. Rangi
6. Jiko  la  mafuta  ya  taa  au  mkaa.
7. Sufuria.
8. Boric  acid.Paraffin  Wax. 

:
VIDOKEZO  MUHIMU :
1. Paraffin Wax :
Hii  inatokana  na  nta  na  sega  ya  nyuki   iliyo  changanywa  na  mafuta  ya  taa.  Ina  rangi  nyeupe  na  katika  utengenezaji  wa  mishumaa  ina  ubora  kuliko  bee  wax.

     *  Bee  Wax   :  Inatokana   na  masega  ya  nyuki   yaliyo  changanywa  na  mafuta  ya  petroli  na  diesel  na  rangi  yake  ni  ya  njano.

2. STEARINE 
Hii  dawa  maalumu  inayo  fanya  mishumaa  iungane  ama  ishikamane.

Mould ( Umbo )  . Mfano  wa  umbo  linalo  weza  kutumika  kutengeneza  mishumaa. Hata  hivyo, unaweza  kutengeneza  umbo  lolote  kwa  kadri  unavyo  taka  " shape "  ya  mishumaa  yako  iwe. 
3. BORIC  ACID  :  Hii  ni  maalumu  kwa  ajili  ya  kuufanya  utambi  usiishe  mapema  na  uwake  bila  kutoa  moshi.

4. RANGI  :  Rangi  nzuri  zinazo  tumika  katika  utengenezaji  mishumaa  ni  rangi  za  chakula  na  nyingi  huwa   ni  za  maji.
Boric  acid  , hii  ni  maalumu  kwa  ajili  ya  kuufanya  utambi  usiishe  mapema  na  kuufanya  uwake  bila  kutoa  moshi.


                              JINSI  YA  KUTENGENEZA

Andaa  mould  (  umbo  lako  )  utakalo  litumia  baada  ya  kuyeyusha  (  paraffin  wax  )  na  kuchanganya  na  michanganyo  yote.

Kwa  Mfano :  (  Kipimo  cha  stearine  )
1. Wax  kilo  moja  -  Stearine  vijiko  vinne  vya  chakula.
2. Wax  nusu  kilo  -  Stearine  vijiko  vinne  vya  chakula
3. Wax  robo  kilo - Stearine  kijiko  cha  chakula.


*  Baada  ya  mould  (  umbo )  kuwa  tayari , chemsha  wax mpaka  iyeyuke  na  itoe  kwenye  vyombo  ambavyo  umetayarisha  na  usubiri  ikauke  ili  uanze  kutoa  mishumaa.

3 comments:

 1. post nzuri,ila wekeni vizuri zaidi. Mafano;boric acid hamjaweka vipimo vyake.
  Nadhani mgeweka step kwa step vipimo na michanganyo yake.

  Good job.

  ReplyDelete
 2. Umetueleza vizuri lkn kwa juu juu tu

  ReplyDelete
 3. Umetueleza vizuri lkn kwa juu juu tu

  ReplyDelete