Total Pageviews

Monday, November 26, 2012

NAFASI ZA UANDISHI WA VITABU VYA KITAALUMA..

RafikiElimu  FOUNDATION   ni  TAASISI  isiyokuwa  ya  kiserikali  (  NGO )  inayo  jihusisha  na  Maendeleo  Ya  Jamii .  Taasisi  kupitiaa   mpango  wake   "  DISTANCE   LEARNING  PROGRAMME"   "  Mpango  Wa  Elimu  Ya  Masafa  Marefu  "   inatangaza  nafasi  za   UTAYARISHAJI  & UANDISHI  WA  VITABU  VYA  KITAALUMA.

SIFA  ZA  MWOMBAJI.

Awe  na  elimu, ujuzi, sifa  na  uwezo  wa  kuandaa na  kutayarisha   muswaada  wa  uandikaji  wa  kitabu   cha  kitaaluma  katika  moja  wapo  kati  ya  masomo  yafuatayo :


1.  Law

2.  Mass  Com  &  Journalism.

3. Community   Development.

4. Business  Administration.

5.  NGO  Studies.

6.  Beauty  &  Therapy   Studies .

7. Hotel  Management  &  Tourism.

8. Physical   Education.

9.  Enterpreneurship   Studies.

10.Vitabu  Vya  Masomo  kwa  Waalimu  Wa  Chekechea.

11. Gender  Studies.

12. Social  Researches

13. HIV/ AIDS  &  Counselling.

14. Environmental  Studies

15.  Refugee  Studies

16. Vitabu  Vya  Masomo  yote  ya  O-Level  kwa  mtaala  wa  masomo  ya  O-LEVEL kwa  miaka miwili.

17. Vitabu  Vya  Masomo  ya  A-LEVEL,  michepuo  ya   ARTS  kwa  mtaala wa  masomo ya  A-LEVEL  kwa  mwaka  mmoja.

MAJUKUMU :  Kuandaa  muswaada  wa  somo  husika  kwa  ajili ya  kuchapwa  kama  kitabu  cha  kutumika  katika  elimu  ya  masafa  marefu.


Tuma  maombi  yako  kwenda  kwa  :
Managing   Director,
RafikiElimu   FOUNDATION.
P.O. Box  35967,
DAR  ES  SALAAM.

Au  unaweza  kutuma  aombi  yako  kwa  njia  ya  barua  pepe  yetu  ambayo  ni  :

rafikielimutanzania@gmail.com.


Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe    07  DESEMBA  2012  .

N.B :  ( MUHIMU  SANA  )  :  Unapotuma  maombi  yako, weka  somo  unalotaka  kuliandikia  muswaada  wa  kitabu  kwenye  kichwa   cha  barua pepe  yako.

Friday, November 16, 2012

SOMO LA TISA : USINDIKAJI WA MAZAO YA NAFAKAMahindi  yaliyo  toka  kuvunwa.
1.   USINDIKAJI  WA   ZAO  LA  MAHINDI :

Ili kuongeza matumizi ya mazao hayo na kudumisha ubora wake ni muhimu teknolojia za
kusindika nafaka zitumike. Usindikaji pia huongeza thamani ya zao.

                            KUSINDIKA MAHINDI

Punje za mahindi hutumika kupika makande na husindikwa kupata unga unaotumika katika
matumizi mbalimbali. Vile vile bidhaa nyingine zinazotokana na mahindi ni mafuta na wanga.

KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA

Kuna aina mbili za unga wa mahindi, unga wa mahindi yasiyokobolewa(Dona) na unga wa
mahindi yaliyokobolewa (Sembe)

 KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA WA DONA

Vifaa
• Mashine ya kukoboa
• Mashine ya kusaga
• Ungo
• Debe
• Mifuko
• Chekeche ya nafaka
Jinsi ya kusindika
• Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia.
• Osha kwa maji safi na salama
• Anika kwenye chekeche safi ili yakauke
• Saga mahindi kupata unga


• Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni, makaratasi yasiyopitisha
unyevu kisha hifadhi katika sehemu safi na kavu

Kumbuka: Kusaga mahindi bila kukoboa hudumisha virutubishi vilivyomo kwenye mahindi na
kupunguza upotevu wa chakula.

UNGA WA MAHINDI YALIYOKOBOLEWA

Jinsi ya kusindika
• Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia
• Koboa na saga
• Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni na ya karatasi isiyopitisha
unyevu.
• Hifadhi kwenye sehemu safi na kavu

Kumbuka:Kusaga mahindi yaliyokobolewa hupunguza virutubishi na wingi wa chakula kwa kiasi
cha asilimia 17 hadi 33.
Matumizi ya unga wa mahindi
Hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile ugali, uji, togwa na vyakula vya watoto.
Pia huchanganywa na shayiri na kutengeneza vinywaji kama vile bia.
Mchele  baada  ya  kukobolewa.
2.  KUSINDIKA MPUNGA
Mpunga husindikwa kupata mchele ambao pia husindikwa kupata unga.
Kusindika mpunga kupata mchele
Vifaa
• Mashine ya kukoboa
• Madebe
• Ungo
• Chekeche
• Vifungashio

Jinsi ya kusindika
• Anika mpunga juani kwa muda wa siku moja kisha uache upoe kwa usiku mmoja ndipo
ukoboe.
• Pepeta na pembua kutoa takataka kabla ya kukoboa
• Koboa kwa kutumia mashine.

Kufungasha
Baada ya kupanga madaraja fungasha kwenye mifuko isiyopitisha unyevu na hifadhi katika
sehemu kavu na safi.

Matumizi ya mchele

Mchele hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile wali, uji, biriani, mseto, pilau, bisi,
tambi na vitafunwa. Chenga za mchele hutmika kwa kutengeneza chakula cha mifugo.


KUSINDIKA MCHELE KUPATA UNGA
Vifaa
• Mashine ya kusaga
• Vifungashio

Jinsi ya kutengeneza
• Saga mchele safi kupata unga
• Fungasha kwenye mifuko safi na kavu isiyopitisha unyevu
• Hifadhi katika sehemu safi na kavu.
Matumizi ya unga wa mchele
Hutumika kupika ugali, uji na vitafunwa. Virutubishi vinavyopatikana kwenye unga wa mchele ni
kama vile vilivyoainishwa kwenye virutubishi vya mchele.


3.  KUSINDIKA MTA M A / UWELE
Punje za mtama na uwele hupikwa makande na husagwa kupata unga.
 KUSAGA MTAMA/ UWELE KUPATA UNGA:
Vifaa
• Mashine ya kusaga
• Ungo
• Chekeche ya nafaka
• Kichanja
• Turubai
• Vifungashio safi

 
Jinsi ya kusaga unga

• Pepeta na kupembua mtama/ uwele ili kuondoa mavumbi na takataka nyingine. Tumia
chekeche au ungo kupepeta na kupambeua
• Osha kwa maji safi kisha anika juani kwenye kichanja au turubai
• Saga kupata unga wa mtama/uwele
• Fungasha kwenye mifuko ya nailoni/ plastiki
• Hifadhi katika sehemu safi na kavu
Matumizi ya unga wa mtama/ uwele
Hupikwa ugali, uji na togwa. Vile vile htumika katika kutengeneza vyakula vya watoto


Ngano.

4.  KUSINDIKA NGANO

Ngano husagwa ili kupata unga
Vifaa
• Vifungashio
• Mashine ya kusaga
Jinsi ya kusaga
• Nyunyuzia maji kwenye ngano
• Koboa na saga ili kupata unga
• W eka kwenye vifungashio safi na visivyopitisha maji
Matumizi
• Unga wa ngano hutengeneza vitafunwa kama vile mikate, chapati, maandazi, tambi na
keki.
• Hutumika katika mapishi mbalimbali

SOMO  LA  KESHO :  USINDIKAJI  WA  MAZAO  YA  MIZIZI.

Wednesday, November 14, 2012

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.

 Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka.

MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI.

* Nanasi.

*  Maji.

* Sukari.

* Amira.

HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA

*  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  )

*  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenye  uzito  wa  kg. 5.

* Chemsha  kwa  muda  wa  dakika  30  kwa  moto  wa  kawaida (  Inashauriwa  kutumia  moto  wa  mkaa  )

* Baada  ya  kupoa   anza kuchachua  kwa  kuweka  amira   vijiko  vinne (  4  )  vya  chakula ,  sukari  vijiko  viwili  vya  chai na  kisha  koroga  kwa  muda  wa  dakika  20.

*  Acha  kwa  muda  wa  dakika  5  ukiwa  una  koroga  kila  siku.


HATUA  YA     PILI.

Baada  ya  siku  tano  kukamilika, chuja  wine  yako  iweke  katika  chombo  cha  kupunguza  gesi  kwa  muda  wa  siku  21.  Baada  ya  siku  21 , wine  yako  itakuwa  tayari, unaweza  kui  hifadhi  kwa  ajili  ya  matumizi.

SOMO LA SABA : UTENGENEZAJI WA WINE YA NDIZI

Wine  ya  Ndizi.
 Wine  ya  ndizi  inatokana  na  ndizi  mbivu.  Aina  yoyote  ya  ndizi  ambayo  inaweza  kuwiva  inaweza  kutumika  kutengeneza  wine.

Ili  wine  yako  iweze  kuwa  na  kilevi  ni  lazima  uichanganye  na  amira, usipoweka  amira  wine  yako  itakuwa  tamu  lakini  isiyokuwa  na  kilevi.

MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NDIZI.

*  Ndizi   zilizo  iva  vizuri.

* Maji

*  Vyombo  vya  kuhifadhia.

*  Amira

* Sukari.


HATUA  ZA  KUFUATA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NDIZI.

                                              HATUA  YA  KWANZA :

*  Chukua   ndizi  kg.3  zilizo  menywa  maganda  na  ambazo  zimeiva  vizuri, katakata   vipande  vidogo  na  weka  katika  chombo  ambacho  utatumia  kuchachulia  wine  yako.


*  Baada  ya  kupata  hivyo  vipande  vidogo  vidogo , vichanganye  kwenye  maji  lita  ( 5 )  na   baada  ya  hapo  chemsha   kwa  muda  wa  dakika  30.

* Acha  mchanganyiko  wako  huo  upoe.

                                                    HATUA   YA  PILI

*  Changanya  mchanganyiko  wa  ndizi  na  sukari  kikombe  kimoja   cha  chai, koroga  kisha  changanya  na  amira   vijiko  vinne (  4  )  vya  sukari, koroga  tena.

*  Acha  kwa  muda  wa  siku  nne,   siku  ya  nne  utakapo  kwenda  kuitazama  wine  yako  utakuta  povu, hii  ina  maana  kuwa  wine  yako  itakuwa  imeanza  kuchachuka   vizuri.

*  Siku  ya  tano  (  5  )  chuja  wine  yako  vizuri  kwa  kutumia  kitambaa  lakini  bila  kufinyanga, iache  wine  imwagike  yenyewe.

                                               HATUA  YA  TATU 

* Iweke   wine  yako  kwenye  chombo  cha  kutolea  hewa  na   kupunguza  gas  kwa  siku  1  mpaka  miezi  3.

*  Baada  ya  siku  21  wine  yako  itakuwa  tayari.

SOMO LA SITA : UTENGENEZAJI WA MANGO PICKLESMango  Pickles MANGO  PICKLES    au    "  ACHARI  YA  EMBE  "  ni  chachandu  inayo  tumika  kunogesha  utamu  wa  chakula.   Malighafi  kuu  katika  utengenezaji  wa  "  MANGO  PICKLES "  ni  embe.

                                  MATAYARISHO

* Embe  zisafishwe  vizuri  kwa  kuosha  vizuri  kwa  kutumia  maji  masafi.
( Embe  zioshwe kabla  hazijamenywa )

* Embe  likatwe  katwe  vipande  bila  kuligusa  kokwa,  vipande  hivyo  viwekwe  kwenye  kichanja  baada  ya  kukatwa  katwa  na  vianikwe   juani  kwa  muda  wa  nusu  saa.

*  Hifadhi  embe  zako  hizo  kwenye  chombo  kisafi, kwa  muda  wa  siku  tano.


                     KUTENGENEZA  MANGO  PICKLES

* Tayarisha  nyanya  robo  kilo, menya  maganda  na  katakata  vipande  vidogo.

* Katakata  vitunguu    viwili   vikubwa.

* Chumvi   vijiko  viwili  vya  chai.

* Vinegar  _  kijiko  kimoja  cha  chai  kwa  ajili  ya  kuifanya  mango  pickle  yako  isiharibike.

* Maji  ya  limao  vijiko  viwili  vya  chai.

Tengeneza   rosti  ya  mchanganyiko  wa  malighafi  zote  zilizo  tajwa  hapo  juu. Baada  ya  kutengeneza  rosti  hiyo, chukua  vipand  vyako  vya  embe na  changanya  na  rosti  yako.

Weka  vipande  vyako  vya  embe  ndani  ya  rosti  hii, kisha  hifadhi  katika   kifungashio  kwa  ajili  ya  matumizi ..

N.B:  Kwa  kiwango  hiki  cha   rosti  una shauriwa  uweke   vipande  vya  embe  vyenye  uzito  wa  kilo  moja.  

NAFASI ZA KU- VOLUNTEER DAR ES SALAAM.


 TANZANIA  SCIENCE  JOURNALISTS  ASSOCIATION,  inazo  nafasi  za  kazi  za  kujitolea     kama  ifuatavyo  :

Requirements for Volunteers
1.)Have interest in writing science stories
2.)Be innovative on science technology and innovation stories
3.)Be committed


                                            MAWASILIANO  YAO :

Email address:tasja_11@hotmail.com
Phone number:+255 715 600 568, +255 784 359555, +255 712 756046
Street address:P.O.BOX 10160
DAR ES SALAAM
TANZANIA - E/AFRICA
Mailing address:P.O.BOX 10160
DAR ES SALAAM,
TANZANIA - E/AFRICA
Contact name:GREYSON MUTEMBEI
Contact title:PROGRAMME PRODUCER

NAFASI ZA KUVOLUNTEER WILAYA MBULU, MANYARA.

Taasisi  ya  SANU  ENGLISH    PRE &  PRIMARY  SCHOOL  ya  Wilayani  Mbulu, mkoani  Manyara  inazo  nafasi  za  kujitolea  kama  ifuatavyo  :

  • 2Teachers – certificate in teaching from any institution
  • A SCIENCE TEACHER,A MATHS TEACHER
  • GRANT FOR CHILDREN DORMOTORIES AND
  • GRAN FOR TEACHERS REMUNARATION FOR 3 YEARS
We would like to have volunteers come for at least one semester   this will  allow for the best quality learning, if volunteers want to travel during the weekend doors are open to go to everywhere in the country Sanu English welcome your participation and idea
Taswira  ya  SANU  ENGLISH  PRE & PRIMARY  SCHOOL.

Maombi  yatumwe  kwa  :

MANAGING  DIRECTOR,
SANU  ENGLISH  PRE  &  PRIMARY  SCHOOLS
P.O.Box   35,
Mbulu  District,
MANYARA. 

proverbfour13@yahoo.com

SIMU  :  +255784 928167

Tuesday, November 13, 2012

NAFASI YA KUJITOLEA BABATI.


Picha  za  matukio  ya  shughuli  mbalimbali  za  Taasisi  ya  LATI  TANZANIA.
Look  After  Them  International,  ni  Taasisi  Isiyokuwa  ya  kiserikali  yenye  makao  yake  wilayani  Babati , mkoani  Manyara,  taasisi  inatangaza  nafasi  moja  ya  kazi  ya  kujitolea  katika  fani    ya   uhasibu.

Sifa:
1. Mwanaume.
2. Atakaye weza kujilipia gharama za chakula.
3.Atakayeweza kufanya kazi si chini ya mwaka mmoja.
4.Creative and Innovative.
5.Mvumilivu.
6.Team builder.
7.Christian.
Kazi:
1.Atapitia sera za fedha na kuziboresha.
2.Atafanya mlinganisho wa kibenki.
3.Ataandaa financial reports ya 2009,2010,2011,2012 by using international standards.
4.Atatoa report na ushauri kwa board.
5.Ataripoti kwa Katibu Mkuu.
6. Ataandaa donor's log book.
7. Atabuni na kutekeleza miradi ya kutunisha mfuko kwa kushirikiana na management.
Facilities.
1.Computer with Internet.
2.Office.
3.Accomodation meals exclusive.
4.Volunteers T-shirt.

N:B.He will be awarded a certificate of volunteering.

Important:
Akiandika mradi mzuri ukapata fedha allowance yake itakuwepo kwa kipindi cha kutekeleza mradi huo.

Tuma  maombi  yako  kupitia  barua  pepe  :     lati.tanzania@yahoo.com
kwenda  kwa 
KATIBU  MKUU,
LOOK  AFTER  THEM  INTERNATIONAL  ( TZ  )
S.L.P   341,
BABATI- MANYARA.

Contacts  : +255782093872, +255753843775

SOMO LA TANO : UTENGENEZAJI WA TOMATO SOUCE.

Maandalizi  ya  utengenezaji  wa  Tomato  Souce.


Tomato  Souce.

MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KWENYE  UTENGENEZAJI  WA  TOMATO  SOUCE.

1. Nyanya            Kg  1.5 (  Kilo  moja  na  nusu  )
2.Vitunguu  Maji.      Vitatu  vilivyo  menywa  na  kukatwa  katwa  vipande.
3. Mafuta  ya  Kupikia     Vijiko  Sita  Vya  Chakula.
4. Sukari                        Vijiko  viwili  vya  chai.
5. Citric  Acid.
6.Vinegar.                          Vijiko  viwili  vya  chai.

HATUA  ZA  KUFUATA  WAKATI  WA  UTENGENEZAJI  WA  TOMATO  SOUCE. 


Tomato  Souce  iliyo  katika  hatua  za  maandalizi 1. Saga  mchanganyiko  wa  malighafi  zote  zilizo  tajwa  hapo  juu  kwa  pamoja  kwa  kutumia  mashine  ya  blender  mpaka  uwe  rojo  rojo.

2. Tenga  jiko  la  mkaa  lenye  moto  wa  wastani, kisha  injika kikaangio  kwenye  moto  halafu  weka  mafuta  ya  kupikia  vijiko  sita   vya  chakula.
3. Mafuta  yakianza  kuchemka , anza  kumimina  mchanganyiko  wako  huo  ndani  ya  kikaango  hicho   huku  ukiwa  una  koroga  upande  mmoja  mpaka  umalize  kuchanganya. Tumia  dakika  15  kufanya  zoezi  hili.

*  Utakapo  ona  mchemsho  wako  umeanza  kuwa  uji  uji, ipua  na  weka kwenye  chombo  safi  tayari  kwa  matumizi.

Monday, November 12, 2012

NAFASI ZA KUJITOLEA GEITA.

Taasisi  ya  BRIGHT  LIGHT  ORGANISATION  ya  Wilayani  GEITA  inatangaza  nafasi  za  kazi  za  kujitolea  kama  ifuatavyo :

Picha  za matukio  ya  shughuli  mbalimbali  za  Taasisi  ya  BRIGHT  LIGHT  ORGANISATION  ya  wilayani  GEITA .1:WALIMU  WAWILI  (ME na KE) ambao wanaweza kufundisha SCIENCE na ARTS,shule  ya  Sekondari.

2:-AFISA  MIRADI " Project  Officer  "  ambaye anaweza kubuni  na  kuandika  miradi  malimbali  yenye  tija  kwa  wafadhili.


HUDUMA  TUTAKAZO  TOA.
 
Sisi  kama taasisi  ya  Bright  Light  Organisation  tutatoa  huduma  ya Chakula na malazi ,na itakuwa vizuri iwapo watakuwa tayari kuishi mazingira ya karibu na kituo chetu ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

Kama  una  sifa  hizo  hapo  juu  na  ungependa  kufanya  kazi  kama  mjitoleaji  katika  maeneo  tajwa  hapo  juu  kwenye  wilaya  ya  Geita,  andika   barua  yako  ya  maombi  kupitia    barua  pepe brightlightorg@yahoo.com


Maombi  yatumwe  kwa :

Mkurugenzi  Mtendaji,
BRIGHT  LIGHT  ORGANISATION,
P.O.Box  648,
GEITA. 

Deadline  ya  kupokea  maombi  ni  tarehe  20  NOVEMBA  2012. 

NAFASI ZA KUJITOLEA SINGIDA

Taasisi  ya  ORPHANS  &  VULNARABLE   CHILDREN  CARE   (  OVCC  )  ya  Mjini  SINDIDA  inatangaza  nafasi  za  kazi  za  kujitolea  kama  ifuatavyo  :


Picha  za  matukio  ya  shughuli  mbalimbali  za  Taasisi  ya OVCC.
 
1.      Miandi Secondary school:-

      Volunteers wa masomo yafuatayo:-
         (i) Physics               2
         (ii) Chemistry           2
         (iii) Biology              2
         (iv) Geography         1
         (v) Basic Mathematics. 2

2.       Puma Secondary School:-

      Volunteers wa masomo yafuatayo:-
        (i) Fnglish                        2
        (ii) Physics                      3
        (iii) Chemistry                  3               
        (iv) Biology                      3
        (v) Basic Mathematics     4

3.      Puma Dispensary:-

    Volunteers wa Taaluma zifuatazo:-
      (i) Taaluma ya Utabibu             8
      (ii) Taaluma ya Kinga ya Afya   8
      (iii) Taaluma ya Uuguzi            8

Jumla wanahitajika voluteers      24 katika Dispensary ya Puma na watakuwa wanafika vijjijini na kukutana na jamii na kufanya kazi.


4.       Utaho Secondary School:-

     Volunteers wa masomo yafuatayo:-
       (i) Basic Mathematics  2
       (ii) Geography             1
       (iii) Biology                 2
       (iv) Chemistry             2
       (v)  Physics.              1

5. Shule  Za  Msingi ;Musambu , Wibia, Matyuku:-
     Masomo yafuatayo:-
        (i) English    2 kwa kila shule
        (ii) Sayansi  2 kwa kila shule

6. Puma Shule ya Msingi
    Volunteers wa masomo yafuatayo:-
        (i) Hesabu      2
        (ii) Kiswahili   1
        (iii) Geography 2
        (iv) History       1
        (v) Tehama       1
        (vi) English       2
        (vii) Sayansi     2

Maombi   yote   yatumwe  kwa  njia  ya  barua  pepe : orphansandvulnerablechildrencare@yahoo.com  ,
kwenda  kwa   ;

Managing  Director,
ORPHANS &  VULNERABLE   CHILDREN  CARE (  OVCC )
P.O . Box   770,
SINGIDA  TANZANIA.

Contact  Person :   Mr. Benard  Sungi  (  OVCC- Coordinator ) 
                              SIMU  : +255756435061.