Total Pageviews

Monday, August 27, 2012

TAARIFA KUHUSU UZINDUZI WA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI.

  Uongozi  wa   RafikiElimu  Foundation,  unapenda   kuwa  julisha    wajasiriamali  wote  walio  jiandikisha  katika   Mradi  Wa  Mafunzo  Ya  Ujasiriamali  Mijini & Vijijini, (  EUMIVI  PROJECT ) kwamba  mradi   utazinduliwa  rasmi  siku  ya   Jumamosi  ya  tarehe  01  Septemba   2012,  kuanzia  saa  nne  kamili  asubuhi   katika    eneo  la  Shule   Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika   eneo  la   Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam.

Mambo  yatakayo  fanyika   katika  siku  ya  uzinduzi  ni  pamoja  na  kuutambulisha  rasmi  mradi  na  kuanza  kutoa  mafunzo  rasmi.    Kwa  wewe  uliye  jiandikisha  unaombwa  kufika  na  kitambulisho  chako,  kalamu, pamoja  na   daftari.


Majina   Ya    Wajasriamali  wote  wa  jijini  Dar  Es  salaam  walio  jiandikisha  katika  awamu  ya  kwanza  ya  mradi  huu  yatatolewa  rasmi  siku  ya  kesho, yani  tarehe  28  Agosti  2012 ( ambayo  ndio  siku  ya  mwisho  kujiandikisha  katika  mafunzo )   saa  kumi  kamili  jioni  hapa  hapa  katika   tovuti  yetu...  Kwa  wajasiriamali  wa  mikoani  mtapewa   taarifa  rasmi  kuhusu  mafunzo  siku  ya  kesho (  tarehe  28  Agosti  2012 )  ifikapo  saa  kumi  kamili  alasiri.  Vilevile  waombaji  wote  mtatumiwa    ujumbe  mfupi  wa  maneno, kuwaita   katika  mafunzo.

Kufika  katika  eneo  la  Shule  Ya  Msingi  Mlimani, kama  unatokea  Ubungo   au  Mwenge , panda  gari  za  Ubungo  Chuo   Kikuu,  shuka  kituo  cha  magari  kinaitwa    UDASA, ukifika  hapo  UDASA  utamkuta  mtu  ambaye  atakupokea  na  kukuelekeza  kilipo  kituo  cha  mafunzo.


TAFADHALI  ATAKAYE  LIPATA  TANGAZO  HILI  AWAFAHAMISHE  NA  WENZAKE.
KWA  MAELEZO  ZAIDI  WASILIANA  NASI  KWA 0763976548   AU  0782405936.

No comments:

Post a Comment