Total Pageviews

Saturday, August 11, 2012

BAJETI YA ELIMU TANZANIA, 2012/2013 ITAMALIZA AU KUPUNGUZA KERO HIZI?

Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Isensa ya wilayani Nkasi wakiwa darasa, darasa hili lina wanafunzi 211, mwalimu hana pa kukaa akifundisha hutoka nje kusubiri watoto wamalize kuandika.
Shule ya msingi Selous iliyopo Namtumbo. Wanafunzi wa darasa la tano wakiwa darasani na mwalimu akifundisha.
Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini.
Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini.
BAJETI ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti 2012. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kama Shule ya Msingi Selous na shule  ya  Msingi Mkapa zilizopo wilayani Namtumbo, mkoani  Ruvuma, Shule ya Msingi Silabu iliyoko wilayani Korogwe, mkoani  Tanga  na Shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi,mkoani  Rukwa pamoja   na baadhi ya shule wilayani Muleba  na  Tanzania  nzima  kwa  ujumla.

Shule hii ipo wilayani Muleba.
Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule. Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?

?
Hiki ni choo cha Shule  ya  Msingi  iliyopo   wilayani Muleba, mkoani  Kagera. Ni msingi  upi  tunaojengea  watoto  wetu  kama  wanajifunza  katika  mazingira  yasiyo  rafiki  kama  haya? 
Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga, Rukwa, Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenyesehemu zinazokatisha tamaa: Wataweza  kweli? Mungu  Ibariki  Tanzania , Mungu  Ibariki  Afrika!

No comments:

Post a Comment