Total Pageviews

Wednesday, August 29, 2012

ORODHA YA MAJINA YA WAJASIRIAMALI WA JIJINI DAR ES SALAAM WALIO JIANDIKISHA KATIKA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI.

Yafuatayo  ni  majina   ya   vijana  wa  kitanzania  walio  jiandikisha  katika  awamu  ya  kwanza  ya   Mradi  wa  Elimu  ya Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  "  EUMIVI   PROJECT. mbao  utaanza  rasmi  siku  ya  jumamosi  ya  tarehe  01  Septemba  2012   kuanzia  saa  nne  kamili  asubuhi  katika  Shule Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika  eneo  la  Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam.  Kwa  jijini  Dar  Es  salaam, mafunzo  yatachukua  siku  tatu, kuanzia  tarehe  01 Septemba  2012  hadi  tarehe 03 Septemba  2012. Baada  ya  hapo mradi  utaendelea  katika  miji  ya Arusha, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Tanga  na Shinyanga

          ORODHA   HII  NI    KWA  WAOMBAJI   KUTOKA  JIJINI   DAR ES  SALAAM.

1.  MIRIAM  SYLLERSAID  MZIRAY
2. OTMARY   CHRISPIN  KIOWI.
3. MONICA   ELIAH  NG'ONA.
4.  SHEBA  SHAABAN.
5. FRIDA  EMMANUEL  MUGARULA.
6. AYUB  G.  KAYOMBO.
7.AMIRI  M.  MAGORWA.
8.  FRANK   KAYUMBA.
9.ELIZABETH   PATRICK.
10.   SHEHA   MOHAMED.
11. ROSEMARY  FAUSTIN  MAOKOLA.
12.  MAGRETH   GERWIN  FAYA.
13. DANIEL   A.  SWILA.
14.  MULIMBA  O.  RUYEMBE.
15. MWAJUMA  SHAMTE.
16.  SAMIA  SELEMANI.
17. MWANTUMU  SELEMANI  KALULU.
18. BEATRICE  MIROBO   CHISANYO.
19. HILDEGATH   HAULE.
20.  JOYCE   MAIGE  MGALAGANZA.
21.  DIANNA   R.  MTAITA.
22.LEOKADIA  KINGAMKONO  (  Tafadhali  Tujulishe  namba  yako  ya  simu  haraka  iwezekanavyo )
23.  MUGANYILE  E.  GABRIEL.
24.REHEMA  WILLIAM.
26.  MAGDALENA   R. SHAYO.
27. IBRAHIM  JUMA  OMAR.
28. SOPHIA  SELEMANI  ISSA. ( Tafadhali  tujulishe  namba  yako  ya  simu  haraka  iwezekanavyo O
29.  VICTORIA   ABDALLAH  MPOMA  (  Tafadhali  tujulishe  namba  yako  ya  simu  haraka  )
30. JANETH  ANDREW.
31. LILIAN  BAHATI  (  Tafadhali  tujulishe  namba  yako  ya simu  haraka  iwezekanavyo )
32.  YUSUFU   SAID  JADI.
33. TABU  RASHIDI   LWASSA.
34. MASUMBUKO  MANG'OMBE  JAMES.
35. HELENA  STEVEN  CHACHA.
36. FADHILI  H.  MOTTO.
37. RAMLA  H. MOTTO.
38. PETER  NGWANDU  MASALU.
_______________________________________________


Kwa  ambao  majina  yenu  yame orodheshwa  hapo  juu, mnatakiwa  kufika  katika  eneo  la  Shule  Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika  Chuo  Kikuu  Cha   Dar  Es  salaam, siku  ya  Jumamosi  ya  tarehe 01  Septemba  2012  saa   tatu  kamili  asubuhi  kwa  ajili  ya  Uzinduzi  wa Mradi  wa  Elimu  ya Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini "  EUMIVI  PROJECT "  ambapo  mafunzo  rasmi  ya  ujasiriamali katika  mradi  huu  yataanza.
Kufika  katika  eneo  la  tukio  (  Shule  Ya  Msingi  Mlimani )  : Panda  gari  za  Ubungo-Mwenge, mwambie  konda  akushushe  kwenye  kituo  kinaitwa   UDASA ukifika  hapo  UDASA   kama  unatokea  Mwenge  , tazama  upande  wako  wa  kushoto  na  kama  unatokea  Ubungo  tazama  upande  wako  wa  kulia ,utaiona  Shule  Ya  Msingi  Mlimani,  hapo  ndipo  yatakapo  kuwa  yanafanyika  mafunzo  haya..

Unashauriwa  kufika  na kitambulisho  chako,    kalamu  pamoja  na  daftari.  Kamera  hazita  ruhusiwa.

N.B: 1.  Kama  wewe    ni  mkazi  wa  jijini  Dar  Es  salaam,  na  ulituma  maombi  ya  kujiunga  katika  mradi  huu lakini  jina  lako  halionekani  hapo  juu. Tafadhali  wasiliana  nasi  haraka  iwezekanavyo  kabla  ya  tarehe  01  Septemba...
       2.  Kama  kuna  majina  ya  waombaji  kutoka  Dar  Es  salaam  yataongezeka, tutayaweka  hapa  bloguni  kabla  ya  tarehe  01  Septemba  2012.
                          KWA  WAOMBAJI  WA  MIKOANI : 
IFUATAYO  NI   RATIBA  YA   UZINDUZI  WA   AWAMU  YA  KWANZA  YA  MRADI  WA  MAFUNZO  YA  UJASIRIAMALI. MIJINI  & VIJIJINI  KATIKA  MIKOA  YA  ARUSHA, MOROGORO, KILIMANJARO, MWANZA, MBEYA  NA  DODOMA.

Kwa  waombaji  wa  mikoani,  ratiba  ya   awamu  ya  kwanza  ya   mafunzo  haya  itakuwa  kama  ifuatavyo :

                      1.   ARUSHA   ,  MOSHI  NA  MOROGORO
                    Mafunzo  yatafanyika    Tarehe   17, 18  na  19,  SEPTEMBA  2012...


                    2.    MWANZA,  MBEYA  NA   DODOMA
     
                Mafunzo  yatafanyika tarehe  27, 28  na  29, Septmba  2012.


Monday, August 27, 2012

TAARIFA KUHUSU UZINDUZI WA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI.

  Uongozi  wa   RafikiElimu  Foundation,  unapenda   kuwa  julisha    wajasiriamali  wote  walio  jiandikisha  katika   Mradi  Wa  Mafunzo  Ya  Ujasiriamali  Mijini & Vijijini, (  EUMIVI  PROJECT ) kwamba  mradi   utazinduliwa  rasmi  siku  ya   Jumamosi  ya  tarehe  01  Septemba   2012,  kuanzia  saa  nne  kamili  asubuhi   katika    eneo  la  Shule   Ya  Msingi  Mlimani  iliyopo  katika   eneo  la   Chuo  Kikuu  Cha  Dar  Es  salaam.

Mambo  yatakayo  fanyika   katika  siku  ya  uzinduzi  ni  pamoja  na  kuutambulisha  rasmi  mradi  na  kuanza  kutoa  mafunzo  rasmi.    Kwa  wewe  uliye  jiandikisha  unaombwa  kufika  na  kitambulisho  chako,  kalamu, pamoja  na   daftari.


Majina   Ya    Wajasriamali  wote  wa  jijini  Dar  Es  salaam  walio  jiandikisha  katika  awamu  ya  kwanza  ya  mradi  huu  yatatolewa  rasmi  siku  ya  kesho, yani  tarehe  28  Agosti  2012 ( ambayo  ndio  siku  ya  mwisho  kujiandikisha  katika  mafunzo )   saa  kumi  kamili  jioni  hapa  hapa  katika   tovuti  yetu...  Kwa  wajasiriamali  wa  mikoani  mtapewa   taarifa  rasmi  kuhusu  mafunzo  siku  ya  kesho (  tarehe  28  Agosti  2012 )  ifikapo  saa  kumi  kamili  alasiri.  Vilevile  waombaji  wote  mtatumiwa    ujumbe  mfupi  wa  maneno, kuwaita   katika  mafunzo.

Kufika  katika  eneo  la  Shule  Ya  Msingi  Mlimani, kama  unatokea  Ubungo   au  Mwenge , panda  gari  za  Ubungo  Chuo   Kikuu,  shuka  kituo  cha  magari  kinaitwa    UDASA, ukifika  hapo  UDASA  utamkuta  mtu  ambaye  atakupokea  na  kukuelekeza  kilipo  kituo  cha  mafunzo.


TAFADHALI  ATAKAYE  LIPATA  TANGAZO  HILI  AWAFAHAMISHE  NA  WENZAKE.
KWA  MAELEZO  ZAIDI  WASILIANA  NASI  KWA 0763976548   AU  0782405936.

Thursday, August 23, 2012

Mitaala shule za msingi inawachanganya wanafunzi – Walimu

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, wakiwa wakati wa mapumziko 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitopeni kutoka Wilaya ya Korogwe. 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, akizungumza na mwandishi wa habari hii 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, wakiwa wakati wa mapumziko
BAADHI ya walimu wa shule za msingi wilaya za Korogwe na Moshi wamelalamikia mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala kwa shule za msingi pamoja na idadi kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa madarasa ya chini, kuwa yamekuwa yakiwachanganya wanafunzi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni walisema mabadiliko ya mara kwa mara kwa mitaala yanayofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi bila maandalizi yamekuwa chanzo cha vikwazo cha kufanya vizuri kwa sekta hiyo.
Akizungumza hivi karibuni na mwandishi wa habari hizi, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Gerezani, mjini Moshi, Khadija Mtui alisema mabadiliko ya mitaala ya mara kwa mara yanawachanganya wanafunzi pamoja na walimu hivyo kuwa kikwazo.
Alishauri kuwepo na maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha walimu ambao ni wadau wakubwa wa sekta ya elimu kabla ya mabadiliko ya mitaala hiyo. Alisema pamoja na hali hiyo mabadiliko ya vitabu vya masomo bila utaratibu mahususi ni tatizo pia katika mafanikio ya sekta hiyo kitaaluma.
“Mabadiliko ya mitaala na mchanganyiko wa vitabu bila utaratibu mahususi ni tatizo, kwa sasa hivi kila shule ina kitabu chake katika somo fulani…hata hivyo licha ya mabadiliko ya mara kwa mara hakuna maandalizi, mimi tangu nimalize chuo 1979 sijaenda semina yoyote wala mafunzo kujiandaa na mabadiliko ya mitaala hii. Hili linachangia pia,” alisema mwalimu Mtui.
Akifafanua zaidi Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Muungano, ya wilayani Moshi, Ashati Elihaki alisema mbali na mchanganyiko juu ya suala la vitabu vya masomo mabadiliko ya mitaala yamegeuza baadhi ya masomo kubaki kama ‘kiini macho’ jambo ambalo ni tatizo kwa walimu.
“…angalia kwa mfano somo kama la Tehama linaloanza kufundishwa darasa la tatu hadi la saba somo hili lipo kinadharia zaidi, hakuna walimu ambao wameandaliwa kufundisha somo hili lakini linatakiwa kufundishwa eti kwa kutumia mwongozo wa mwalimu kimsingi hii si sawa,” alisema Elihaki.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni ya Mjini Korogwe, Theodolph  Karigita alisema tofauti na ilivyokuwa hapo awali mitaala ya sasa imevurugwa kiasi kikubwa jambo ambalo linawachanganya walimu na hata wanafunzi hivyo kushindwa kufanya vizuri.  
“…Mitaala imevurugwa sana, kunamchanganyiko wa masomo nadhani unakumbuka kuna kipindi baadhi ya masomo yaliunganishwa kama Jiografia, Historia na Uraia wakaita maarifa ya jamii…kipindi hiki wanafunzi walifanya vibaya sana hivyo ikabadilishwa sasa watoto wanafanya vizuri tofauti na awali,” alisema Karigita.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lwengera Darajani, Youze Mbwambo alisema idadi kubwa ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu ni chanzo kingine cha wanafunzi hao kufanya vibaya kwani wamekuwa wakibebeshwa mzigo pasipo sababu za msingi.
Akizungumzia hoja hizo zilizotolewa na baadhi ya walimu, Ofisa Elimu Taaluma, Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Elius Mkwizu alisema mabadiliko yanayofanywa na wataalamu hufanywa kwa malengo mazuri licha ya kuwepo na changamoto kadhaa maeneo tofauti

Saturday, August 11, 2012

BAJETI YA ELIMU TANZANIA, 2012/2013 ITAMALIZA AU KUPUNGUZA KERO HIZI?

Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Isensa ya wilayani Nkasi wakiwa darasa, darasa hili lina wanafunzi 211, mwalimu hana pa kukaa akifundisha hutoka nje kusubiri watoto wamalize kuandika.
Shule ya msingi Selous iliyopo Namtumbo. Wanafunzi wa darasa la tano wakiwa darasani na mwalimu akifundisha.
Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini.
Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini.
BAJETI ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti 2012. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kama Shule ya Msingi Selous na shule  ya  Msingi Mkapa zilizopo wilayani Namtumbo, mkoani  Ruvuma, Shule ya Msingi Silabu iliyoko wilayani Korogwe, mkoani  Tanga  na Shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi,mkoani  Rukwa pamoja   na baadhi ya shule wilayani Muleba  na  Tanzania  nzima  kwa  ujumla.

Shule hii ipo wilayani Muleba.
Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule. Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?

?
Hiki ni choo cha Shule  ya  Msingi  iliyopo   wilayani Muleba, mkoani  Kagera. Ni msingi  upi  tunaojengea  watoto  wetu  kama  wanajifunza  katika  mazingira  yasiyo  rafiki  kama  haya? 
Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga, Rukwa, Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenyesehemu zinazokatisha tamaa: Wataweza  kweli? Mungu  Ibariki  Tanzania , Mungu  Ibariki  Afrika!