Total Pageviews

Tuesday, July 31, 2012

NAFASI ZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

RafikiElimu   Foundation     wanatangaza  nafasi za  mafunzo  ya  ujasiriamali .  Mafunzo  yatakayo  tolewa  ni  pamoja  na  :
1.   Kutengeneza  sabuni
2.  Kutengeneza    chaki
3.Kutengeneza  mishumaa.
4.Kutengeneza   viatu  vya  ngozi.
5. Kutengeneza  mkaa  kwa  makaratasi.
6. Kutengeneza  batiki.
7. Uokaji  mikate
8. Usindikaji  wa   vyakula  na  vinywaji  pamoja  na
9.  Uongozi  wa   biashara.

WALENGWA   WAKUU  WA  MAFUNZOSIFA  ZA   WASHIRIKI
Ili  uweze  kupata   nafasi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  unatakiwa  uwe  na  sifa  zifuatazo:
1.  Uwe  raia  wa  Tanzania.
2. Uwe  na  umri  wa  kuanzia  miaka  16  na kuendelea.
3. Uwe  unajua  kusoma  na  kuandika .

ADA  YA  KUSHIRIKI  KATIKA  MAFUNZO

Ada  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  ni  shilingi   Elfu  Ishirini  na  Tano  Tu (  Tshs.  25,000/=)

MALIPO  YA  ADA
Malipo  ya  ada  ya  mafunzo  yafanyike  kupitia   CRDB  BANK,  Account  number 0152395997900 ,   Jina  la  Akaunti  ni    RAFIKI  ELIMU  FOUNDATION.


             Malipo  yafanyike  kabla  ya  tarehe  28 Agosti  2012

            TAREHE  YA      KUANZA  KWA  MAFUNZO
 Mafunzo  yataanza  rasmi  siku  ya  tarehe  01  Septemba  na  yatafanyika  katika  vituo  vya   Dar  Es  salaa,  Arusha, Moshi, Mwanza, Tanga, Morogoro,Mbeya   na  Dodoma.
              
Kujiandikisha   katika  mafunzo  haya,  tuma  barua  yako  ya  maombi  ambatanisha   na    nakala  ya  risiti  ya  malipo  ya  ada  ya  mafunzo    kwenda  kwa  :
Mkurugenzi  Mtendaji,
RafikiElimu   Foundation,
S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.


Mwisho  wa    kupokea    maombi  ni  tarehe   28 Agosti  2012.

KUTOKA TUNDUMA : MAANDAMANO YA WANAFUNZI YASABABISHA VURUGU, POLISI WALAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI..

Wanafunzi na wananchi wakiwa wanachoma baadhi ya Maeneo Tunduma 

 Wananchi wa Tunduma wakiwa wanashuhudia Live tukio la wanafunzi wa shule za Msingi Tunduma walipo goma
 Njia ya Kuelekea Boda la Tunduma ikiwa imefungwa
Wananchi wa Tunduma wakiwa wanashuhudia Live tukio la wanafunzi wa shule za Msingi Tunduma walipo goma  

 KUTOKA  WILAYANI  TUNDUMA  :  Maandamo  ya  wanafunzi  yasababisha  vurugu , polisi  walazimika  kutumia    mabomu  ya  machozi  kutawanya  maandamo  ya  wanafunzi.
PICHA  NA  HABARI  ZOTE  NI  KWA  MUJIBU  WA  ;  WWW.MBEYAYETU.BLOGSPOT.COM .
Kutoka  RafikiElimu :  Tunaiomba  serikali  imalize  mgogoro  huu  haraka  iwezekanavyo  ili  wanafunzi  warudi  darasani  na  kuendelea  na  masomo  yao  kama  kawaida. Mungu  Ibariki  Tanzania, Mungu  Ibariki  Afrika.

KUTOKA SHULE YA MSINGI VWAWA ILIYOPO MANISPAA YA MBEYA, WANAFUNZI WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA WILAYA

Wanafunzi wa shule za msingi Vwawa wakiwa wanapiga vidumu huku wakielekea ofisi ya mkuu wa wilaya ni Baada ya walimu kugoma.
Wanafunzi  wa  Shule  ya  msingi  Vwawa  iliyopo  katika  manispaa  ya  Mbeya  wakiandamana  kuelekea  katika  ofisi  ya  Mkuu  wa  Wilaya   ya  Mbeya   .
Kufuatia  mgomo  wa  walimu  ulioandaliwa  na  Chama  Cha  Waalimu  Tanzania, " CWT "   kuanzia  tarehe  30 Julai  2012    kwa  muda  usiojulikana  hadi  hapo  serikali  itakapo   timiza  madai  yao, wanafunzi  wa  Shule  Ya  Msingi  Vwawa  iliyopo  katika  manispaa   ya  Mbeya, waamua  kuandamana   hadi  katika  ofisi  ya  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Mbeya,  kuishinikiza  serikali   kuwatimizia  walimu  madai  yao  ili  waweze  kuendelea   na  masomo  yao.  Picha  na  habari   kutoka   :  www.mbeyayetu.blogspot.com

KILICHOJIRI KWENYE MGOMO WA WALIMU MKOANI MBEYA

Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi muungano akiwa nje ya shule akichezea mchanga maana walimu wamegoma  
Wanafuzi wapo makini kumsikiliza mwanafunzi mwenzao
Wanafanzi wa darasa la saba shule ya msingi Meta wakiendelea kupeana mazoezi ya masomo mbalimbali baada ya waalimu wao kugoma kuingia madarasani 
Shule ya msingi Meta

MGOMO WA WAALIMU UNAVYO WAATHIRI WANAFUNZI

Juu  wanafunzi  wa  shule  za  msingi   Ipembe, Nyerere, na  Unyankindi  zilizopo  katika  manispaa  ya  Singida  wakiwa  katika  maandamano.  

Mwanafunzi  akiwa  anawafndisha  wanafunzi  wenzake  baada  ya  walimu  kugoma. Hii  imetokea  huko  mkoani  Mbeya  siku  ya   jana  tarehe  30  Julai  2012. Picha  kwa  hisani  ya  MJENGWA  BLOG
Mgomo  uiso  na  kikomo  ulio  andaliwa  na  Chama  Cha  Waalimu  Tanzania   ( CWT )  ambao  umeanza  rasmi  siku  ya    tarehe  30  Julai  2012   kwa  muda  usiojulikana  hadi  hapo  serikali  itakapo  sikiliza  matakwa  ya  waalimu, umekuwa  na  athari  kubwa  sana  kwa  wanafunzi. Waathirika  wakuu  wa  mgomo  huu  ni  wanafunzi  ambao  wanajiandaa  na  mitihani  ya  taifa  ambayo  inakaribia   kuanza  kufanyika  nchi nzima , mfano  darasa  la  saba  nakadhalika. Sisi  kama  RafikiElimu   Foundation  tunaiomba    serikali   imalize  mgogoro  huu  haraka  iwezekanavyo   ili  watoto  wetu   waweze  kuendelea  na  masomo  yao  kama  kawaida.  Mungu  Ibarika  Tanzania, Mungu  Ibariki  Afrika.

Monday, July 30, 2012

NAFASI ZA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

RafikiElimu   Foundation     wanatangaza  nafasi za  mafunzo  ya  ujasiriamali .  Mafunzo  yatakayo  tolewa  ni  pamoja  na  :
1.   Kutengeneza  sabuni
2.  Kutengeneza    chaki
3.Kutengeneza  mishumaa.
4.Kutengeneza   viatu  vya  ngozi.
5. Kutengeneza  mkaa  kwa  makaratasi.
6. Kutengeneza  batiki.
7. Uokaji  mikate
8. Usindikaji  wa   vyakula  na  vinywaji  pamoja  na
9.  Uongozi  wa   biashara.

WALENGWA   WAKUU  WA  MAFUNZOSIFA  ZA   WASHIRIKI
Ili  uweze  kupata   nafasi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  unatakiwa  uwe  na  sifa  zifuatazo:
1.  Uwe  raia  wa  Tanzania.
2. Uwe  na  umri  wa  kuanzia  miaka  16  na kuendelea
3. Uwe  unajua  kusoma  na  kuandika .

ADA  YA  KUSHIRIKI  KATIKA  MAFUNZO

Ada  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  ni  shilingi   Elfu  Ishirini  na  Tano  Tu (  Tshs.  25,000/=)

MALIPO  YA  ADA
Malipo  ya  ada  ya  mafunzo  yafanyike  kupitia   CRDB  BANK,  Account  number 0152395997900 ,   Jina  la  Akaunti  ni    RAFIKI  ELIMU  FOUNDATION.


             Malipo  yafanyike  kabla  ya  tarehe   28  Agosti  2012

            TAREHE  YA      KUANZA  KWA  MAFUNZO
 Mafunzo  yataanza  rasmi  siku  ya  tarehe  01  Septemba  na  yatafanyika  katika  vituo  vya   Dar  Es  salaa,  Arusha, Moshi, Mwanza, Tanga, Morogoro,Mbeya   na  Dodoma.

Kujiandikisha   katika  mafunzo  haya,  tuma  barua  yako  ya  maombi  , ikiambatana  na  nakala  ya  cheti  chako  cha  kuzaliwa  ama   nakala  ya  kadi ya  mpiga  kura, pamoja  na  nakala  ya  risiti  ya  malipo  ya  ada  ya  mafunzo    kwenda  kwa  :
Mkurugenzi  Mtendaji,
RafikiElimu   Foundation,
S.L.P  35967,
Dar  Es  salaam.


Mwisho  wa    kupokea    maombi  ni  tarehe   28  Agosti  2012.
                                    

Tuesday, July 3, 2012

Rafiki Elimu Foundation Yawalipia Ada Yatima Mia Moja Kumi na Tano wa Kike shule za skondari Vijijini.

Katibu  Mkuu  wa  Taasisi  ya  Rafiki  Elimu  Foundation, Bwana  Omary  Baraka  Mbwetom (  wa  mwisho  waliosimama )  akiwa  katika  picha  ya  pamoja na  baadhi  ya  wanafunzi   na mwalimu wa    Shule  Ya  Sekondari  Ya   Kisaza  iliyopo  Wilayani  Handeni  Mkoani  Tanga.
Wanafunzi  wa  Shule  ya  Sekondari  Pangambili  iliyopo  wilayani  Handeni  mkoani  Tanga  wakilima.
Wanafunzi  wa  Shule  ya  Sekondari  Pangambili  iliyopo  wilayani  Handeni  mkoani  Tanga. 
Wanafunzi  wa  Shule  ya  Kwaludege  Sekondari  wakichota  maji  bwawani  kwa ajili  ya  matumizi mbalimbali.
Wanafunzi  wa  Shule  Ya  Sekondari  Kisaza, iliyipo  wilayani  Handeni  mkoani  Tanga.
Kabuku  Secondary  School, Handeni, Tanga.
Wanafunzi  wa  Kabuku  Sekondari  School, iliyipo  wilayani  Handeni  mkoani  Tanga.
Shule  ya Sekondari  Kwaludege  iliyopo  wilayani  Korogwe, mkoani  Tanga.
Wanafunzi  wa  Shule  ya Sekondari  Kwaludege  wakiwa  katika  picha  ya  pamoja  na  Katibu  Mkuu  wa  Rafiki  Elimu  Foundation  pamoja  na  walimu  wa  shule  hiyo.
Wanafunzi    yatima  wa  kike  na  wanaoishi  katika  mazingira   magumu  wapatao  mia  moja  kumi  na  watano (  115 )  wanao soma    katika  shule  za  sekondari  za   Kwaludege  Secondary  School,   Pangambili  Secondary  School,  Kabuku  Secondary  School   pamoja  na  Kisaza  Secondary  School  zilizopo  katika  wilaya  za  Handeni  na  Korogwe Mkoani  Tanga. wamefanikiwa  kupata  udhamini  wa  kusomeshwa   kwa  kulipiwa ada  ya  shule  pamoja  na   vifaa  vinginevyo  muhimu  katika  masomo kama  vile  vitabu  vya ziada  na  kiada.
Udhamini huo, umetolewa  na  Asasi  Isiyokuwa  ya  Kiserikali  iitwayo  "  Rafiki  Elimu  Foundation " ya jijini  Da  Es  salaam  kupitia  mradi  wake  "  Elimisha  Msichana  Project "  uliolenga  katika  kutoa  msaada  wa  kuwasomesha  wanafunzi  wa  kike  wanao  soma  katika  shule  za  sekondari  zilizopo maeneo  ya vijijini  na  ambao wanaishi  katika  mazingira  magumu( mfano  watoto  yatima, na  wale  wenye wazazi  wazee  ama  walemavu ) kwa  kuwalipia  ada  pamoja  na  kuwapatia vifaa vingine  muhimu  katika  masomo  kama  vile  vitabu  vya  ziada  na  kiada. Walengwa  wakuu  katika  mradi   huu  ni  wanafunzi  wa  kike  katika  shule  za  sekondari  zilizopo  maeneo  ya  vijijini  na  ambao wanaishi  katika  mazingira  magumu, mfano yatima, wenye  wazazi  wazee  sana  na  walemavu.

Akiongea  na   waandishi  mbalimbali  wa  habari, Katibu  Mkuu  wa  Taasisi  ya  Rafiki  Elimu  Foundation,  Bwana, Omary  Baraka  Mbweto, amesema  yakuwa , lengo  la  mradi  ni  kuhakikisha  wanawasaidia  wasichana  elfu  tano  wanaosoma  katika  shule  za  sekondari  zilizopo  vijini    na  wanaoishi  katika  mazingira  magumu  katika   mikoa  yote  ya Tanzania  Bara, ambapo  kwa  kuanza    taasisi  yake  imeanza  na  kuwalipia  ada  za  masomo  pamoja  na  vifaa  mbalimbali  vya  shule  wanafunzi  wapatao  mia  moja  na  kumi na  tano  katika  wilaya  ya  Handeni  ambayo  ipo  katika  mkoa  wa   Tanga.

Katibu  Mkuu  wa  Rafiki  Elimu  Foundation (  Wa  Pili  kutoka  kulia, waliosimama  ) akiwa na  wanafunzi  wa  Shule  ya  Sekondari  Kwaludege, iliyopo  Handeni, Mkoani  Tanga  ambao  wanafadhiliwa  na  Taasisi  ya  Rafiki  Elimu  Foundation. Wa  kwanza kulia ( waliosimama/aliye  vaa  shati  la  buluu ) ni  Mwalimu  katika  shule  hiyo  ya  sekondari.
" Mradi  huu, hautaishia hapahapa   Handeni, Tanga  bali  utakuwa  ni  mradi   wa  nchi  nzima, baada  ya  hapa  tutaelekea  wilayani Manyara  ambapo  tunaenda  kufanya  utafiti   katika  wilaya  ya  Babati  na kutoa  msaada  wetu huo,  kabla  ya  kuelekea  katika  wilaya  za  Kondoa  ( Dodoma )    Arumeru (  Arusha  ).  Mkuranga, Rufiji, Kisarawe  na  Mafia (  Pwani ).  Alisema   Ndugu  Mbweto.   " Tukimalizana  na  wilaya  hizo  tutaelekea katika wilaya  nyinginezo  za  Tanzania  Bara " aliongeza.

Bwana  Omary  Mbweto  alisema  kuwa,  ili  kuhakikisha  kuwa  wanafunzi  wanao saidiwa  katika  mradi huu ni  wale wenye  uhitaji  kweli, yani yatima,  watoto wenye  wazazi  wazee  sana  ama  walemavu, taasisi  yake  imekuwa  makini  mno  kwa  kuhakikisha  kuwa   nyaraka zote  muhimu  zinazo  thibitisha  kuwa  mwanafunzi  husika    ni  yatima   na  ama  ana  ishi  katika  mazingira  magumu.

Mradi  wa  Elimisha  Msichana  Project  mbali  na  kuwalipia  ada  na   mahitaji  muhimu  ya  shuleni  kama  vile vitabu  na   kiada  na  ziada  wanafunzi wa kike  yatima  wanaoishi  katika mazingira  magumu  waliopo  katika  shule  za  sekondari  zilizopo  katika  maeneo  ya  vijijini  nchini  Tanzania, pia  umelenga  kutoa  elimu  kwa watanzania  wote  kuwahasisha  kujenga  utamaduni wa  kuwasomesha  watoto wa  kike, na  yatima  wanaoishi  katika  mazingira  magumu.

Mbali  na  kujihusisha  na  maendeleo  ya  elimu  nchini  Tanzania,  taasisi ya  Rafiki  Elimu Foundation   inahusika  na  kutoa  msaada  wa  kisheria  kwa   watu mbalimbali  wenye  matatizo  ya  kisheria  lakini  hawana  uwezo  wa  kumudu  gharama  za  mawakili, huku  kipaumbele kikiwekwa  zaidi  kwa  wanawake, walemavu, wazee  na  katika masuala  ya  elimu.